Nenda kwa yaliyomo

Utao

Kutoka Wikipedia, kamusi elezo huru
Utao
道教 (Dàojiào)

ukubwa_wa_picha
Alama ya Yin na Yang, ishara ya Utao

Uainishaji ya Kidharma
Maandiko Tao Te Ching
Zhuangzi
Daozang
Teolojia Inaweza kuwa Upanthestiki, Upolithestiki, au Uathesti kulingana na madhehebu
Eneo Hasa China, Taiwan, Hong Kong, Vietnam, na Diaspora ya Kichina
Lugha Kichina cha Klasiki, Lugha mbalimbali za Kiasia
Mwaasisi Laozi (kulingana na mapokeo)
Asili Karne ya 4 KK, China ya Kale
Ibada Kutafakari, Ibada kwa mababu, Mazoezi ya Qi Gong, Ibada za hekalu
Wafuasi Takriban milioni 12-20 (idadi halisi haijulikani kwa usahihi)

Utao (pia: udao) ni aina ya imani katika nchi ya China inayoitwa wakati mwingine falsafa na wakati mwingine dini.Asili yake ni katika karne ya 4 KK wakati mzee Laotze alipoandika kitabu cha Tao te king. Mafundisho yake ni msingi wa Utao.Nembo yake ni alama ya taijitu inayojulikana zaidi kama yin-yang inayoonyesha jinsi gani vilivyo kinyume ni umoja.

Pamoja na Ukonfusio na Ubuddha ni moja ya imani tatu zilizoathiri na kuumba utamaduni wa China. Mafundisho yake huonekana katika Siasa, uchumi, sanaa, falsafa, fasihi, chakula, tiba, kemia, jiografia na elimu ya vita.

Tao au Dao kiasili ni neno la Kichina la kutaja "njia". Katika Utao imekuwa njia ya kutaja nguvu inayoratibu ulimwengu. Wafuasi wa Utao huamini ya kwamba hakuna maneno ya kibinadamu yanayoweza kueleza tao yenyewe. Kwa hiyo wanaona umuhimu wa kufuata utaratibu wa maisha badala ya majadiliano ya kinadharia. Tao ina nia yake na mtu anatakiwa kwenda sambamba iwezekanavyo na mwendo asilia wa maisha.

Mafundisho yake hukazia sifa za huruma, upole na unyenyekevu.

Watao wanaokazia upande wakidini wanatafuta raha ya milele. Katika imani yao kuna miungu mingi kwenye ngazi mbalimbali ya enzi. Miungu wa juu ni "watatu walio safi".

Wakati wa ukomunisti mkali chini ya Mao Zedong utao uligandamizwa pamoja na dini zote na mahekalu mengi yaliharibiwa. Wamonaki na makuhani walifungwa gerezani, wengine kuuawa na kulazimihswa kuacha kazi yao. Lakini imani iliendelea kwa siri. Leo hii kuna makadirio ya kwamba labda Wachina milioni 80 hufuata tena Utao pamoja na wengine nje ya Jamhuri ya Watu wa China kama huko Taiwan, Singapur na penginepo.

Makala hii kuhusu mambo ya dini bado ni mbegu.
Je, unajua kitu kuhusu mada hii kama historia yake au uenezi wake?
Labda unaona habari katika Wikipedia ya Kiingereza au lugha nyingine zinazofaa kutafsiriwa?
Basi unaweza kuisaidia Wikipedia kwa kuihariri na kuongeza habari.